Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Spika atangaza maamuzi magumu wabunge wa Chadema

Thu, 7 May 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

SPIKA Job Ndugai ametangaza uamuzi ngumu dhidi ya wabunge wa Chadema waliotii maagizo ya Mwenyekiti wao Freeman Mbowe, kutohudhuria vikao vya bunge na kujitenga.

Aidha, amewataka kurejesha zaidi ya Sh. milioni 110.1 walizolipwa kwa wiki mbili kwa ajili ya kuhudhuria vikao vya bunge na iwapo hawatafanya hivyo watakamatwa na vyombo vya ulinzi na usalama.

Spika Ndugai ameyasema hayo wakati akihairisha Bunge, mara baada ya kupitisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

Amesema anashangazwa na kusikitishwa na agizo la Mbowe kama Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani, kuwalekeza asihudhurie vikao kwa wiki mbili.

“Nimeshangazwa sana na tangazo lile na nimesikitishwa sana kwa sababu hana mamlaka ya kuitisha utoro na mgomo kwa wabunge,”amesema

Amesema taarifa alizonazo wabunge hao wanazurura na kwamba barua ya Mbowe siyo halali na hawataitambua na haina nafasi kwa bunge hilo.

“Wabunge hao (Chadema) kokote waliko warudi haraka kuendelea na kazi zao, watakaondelea na mgomo wajue baada ya wiki mbili hawatapokelewa bungeni isipokuwa kama watapima corona na kupata vyeti rasmi kabla ya kukanyaga geti la bunge na hayo ndiyo maelekezi,”amesema

Kwa mujibu wa Spika, wabunge hao wakati wanaondoka walishalipwa fedha za kujikimu kuanzia Mei mosi hadi 17,jumla ya Sh. milioni 110.16 na kwamba waliendelea na vikao hawatadaiwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live