Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Spika Ndugai, avijia juu vyombo dola sakata la Askofu Gwajima

SPIKA Wa Bunge Job Ndugai?fit=600%2C383&ssl=1 Job Ndugai, Spika wa Bunge la Tanzania

Tue, 31 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Spika Bunge, Job Ndugai, ameviijia juu Vyombo vya Dola nchini kwa kushindwa kumchukulia hatua za kisheria, Mbunge wa jimbo la Kawe, Josephat Gwajima kwa kutoa matamshi yenye kulidhalilisha bunge na kuchoinganisha muhimili wa Bunge na Serikali.

Ndugai ametoa kauli hiyo wakati wa uhitimishaji wa Ripoti ya Kamati ya Bunge ya Maadili, iliwasilishwa Bungeni hapo mapema hii leo kuhusu maamuzi yaliyofikiwa juu ya sakata hilo.

"Mnavyokwenda sio, kutumia platform ya dini kuhamasisha watu, mtusikilize kesho mtasikia mabomu!!!...hii haiwezi kwenda hivi, Mawaziri mnashambuliwa ,Vyombo vya dola vinasema aaanh, sisi tunasubiri tuone jinai ,unasubiri uambiwe na nani?, we mwenyewe huoni".Spika Ndugai

Gwajima alifikishwa mbele ya Kamati hiyo kujibu Hoja alizozitoa kuhusu Chanjo ya UVIKO -19, iliyokinzana na msimamo wa Serikali, hata hivyo ripoti ya Kamati imeeleza kuwa Mbunge huyo alishindwa kutoa vithibitisho kutetea hoja zake licha ya kujinadi kwa mapana akiwa kanisani kwake kuwa anao ushahidi wa kutosha kujitetea kuhusu kauli zake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live