Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Siri ya uteuzi wa timu Nchimbi CCM

Siri Ya Uteuzi Wa Timu Nchimbi CCM Siri ya uteuzi wa timu Nchimbi CCM

Thu, 4 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Sasa ni rasmi kwamba timu atakayofanya nayo kazi kwenye sekretarieti, Katibu mpya wa Chama cha Mapinduzi, Dk Emmanuel Nchimbi imekamilika.

Hii ni baada ya mabadiliko yaliyofanywa jana na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), yakiwaondoa makada waliokuwa kwenye sekretarieti iliyokuwa chini ya Daniel Chongolo, aliyejiuzulu Novemba mwaka jana.

Kama ambavyo Nchimbi aliingia ikaelezwa na mkakati wa kujipanga na uchaguzi mkuu, vivyo hivyo, hata kwa timu yake hiyo iliyotangazwa jana imeelezwa hivyo na wasomi wa masuala ya siasa, kuwa inalenga uchaguzi wa Serikali za mitaa mwaka huu na uchaguzi mkuu wa mwakani.

Mambo mengine yanayotajwa kuchagiza mabadiliko hayo kwa mujibu wa wanazuoni hao ni kukisafisha chama hicho, huku wengine wakisema hawatarajii mambo mapya katika safu hiyo mpya iliyopangwa.

Wasomi hao wamesisitiza kuwa hatua hiyo imelenga kuhakikisha sekretarieti chini ya Balozi Nchimbi inakuwa na safu inayoendana na yenye muunganiko utakaochagiza ufanisi katika utendaji wa chama hicho.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live