Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Silinde awashangaa wanaoshangilia bajeti

9560 Silinde+pic TZWeb

Wed, 20 Jun 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Mbunge  wa Momba (Chadema), David Silinde amesema wakati wameandaa bajeti mbadala ya kurasa 521 ikikataliwa, Serikali imekataa kuyasikia maoni yao na kubaki kushangilia bajeti ambayo haitekelezeki.

Silinde akichangia Bajeti ya Serikali bungeni leo Juni 19, 2018 amesema Waziri wa Fedha na Mipango, Dh Philip Mpango asipokuwa makini, “asipodhibiti Deni la Taifa tutakufa.”

Amesema mwaka jana tulipopitisha bajeti kama hii hii, nakumbuka makofi tuliyopiga kuwa ni bajeti nzuri, tukajenga hoja nzuri kama vile sisi hatueleweki.

Silinde amesema, “ndiyo maana siku ya Alhamisi, wakati waziri (Mpango) anawasilisha Spika (John Ndugai) mwisho akasema ni mapendekezo si bajeti. Mwaka jana mliyoyaahidi hayakutekelezwa, kwa bajeti hii ni kukiri kushindwa, kwa mara ya kwanza, unaona ni bajeti ya kukiri kushindwa na kuomba msaada.”

“Tumekuletea hotuba ya kurasa 521 umekimbia, unataka nini sasa,” amehoji Silinde ambaye pia ni Waziri kivuli wa Fedha na Mipango

Naye Mbunge wa Mufindi Kaskazini (CCM), Mahmoud Mgimwa amesema Tanzania ya viwanda haiwezi kutekelezeka kama sekta ya kilimo haitapewa kipaumbele kwa kutengewa fedha za kutosha.

“Yako mambo mazuri ambayo yapo katika hii rasimu ya bajeti lakini eneo la kilimo linaajiri Watanzania wasiopungua asilimia 66.6 na Dk (Philip) Mpangp (Waziri wa Fedha na Mipango)  anajua hili,” amesema Mgimwa na kuongeza:

“Lakini ukiangalia bajeti yake hairidhishi kabisa, Dk Mpango liangalie hili, tunapaswa kuweka fedha, katika eneo hili kuna ajira, chakula na malighafi zitakazotumika katika viwanda.”

Amesema tusipowekeza vizuri katika eneo la kilimo, “tutakwendaje katika uchumi wa viwanda, ukiangalia wenzetu wa Afrika Mashariki na Kati, asilimia 10 ya bajeti nzima ndiyo wametenga katika kilimo, sisi hatuijatenga hata asilimia tatu.”

Chanzo: mwananchi.co.tz