Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Silinde, Mbene waanguka, Hasunga, Mulugo wapeta maoni

2bd2bbe70b84dcc230bd180e96d0d448 Silinde, Mbene waanguka, Hasunga, Mulugo wapeta maoni

Tue, 21 Jul 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

ALIYEKUWA Mbunge wa Momba, David Silinde na aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Ileje Janet Mbene wameangushwa kwenye kura za maoni kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoani Songwe.

Wakati huo huo, Waziri wa Kilimo ambaye pia alikuwa Mbunge wa Vwawa, Japhet Hasunga na Mbunge wa Jimbo la Songwe Philpo Mlugo wameibuka washindi kwenye majimbo yao kwa kushinda kura nyingi na kuwaacha mbali wapinzani wao.

Sililinde aliyekuwa Mbunge wa Momba kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) aligombea Jimbo la Tunduma kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) baada ya kuhamia hivi karibuni, ameshika nafas ya pili kwa kupata kura 118, akiwa nyuma ya Aden Mwakyonde aliyeibuka mshindi kwa kura 250 na nafasi ya tatu ikishikiliwa na Daines Sichalwe kwa kupata kura 20.

Kwa upande wa Ileje, Wilman Ndile aliibuka mshindi kwa kupata kura 169,akifuatiwa na Geofrey Msongole kura 104, Joel Kaminyoge kura 73 na aliyekuwa Mbunge wa wa Jimbo hilo Janet Mbene akiambulia kura 38 nafasi ya nne.

Jimbo la Vwawa, Hasunga aliibuka mshindi kwa kujipatia kura za maoni 552 kati ya kura 723 zilizopigwa, wengine ni Aliyekuwa mwenyekiti wa Halmashauri ya Mbozi Elick Minga kura 129 na Dismas kura tisa.

Kwa upande wa Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Songwe la Philipo Mlugo ameibuka mshindi kwa kupata kura za maoni 441, anayefuatia Philemon Msomba akipata kura 241 na Maria Bilia akipata kura 49.

Jimbo la Mbozi George Mwenisongole be ameshinda kwa kupata kura za maoni 200, Charles Chenza kura 126 na Mgula kura 72.

Kwa upande wa Jimbo la Momba uchaguzi haujafanyika kutokana na changamoto ya wajumbe wakupiga kura kuchelewa kufika kutokana na jeografia ya Jimbo hilo.

Kutokana na changamoto hiyo uchaguzi uliahirishwa na kusogezwa siku ya leo julai 21 mwaka huu 2020.

Chanzo: habarileo.co.tz