Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shonza alalamikia wabunge viti maalum kutoshirikishwa kamati za fedha

Wabungepiic Data Shonza aliwahi kuwa Naibu Waziri wa Habari wakati wa Utawala wa Mwendazake

Tue, 19 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Juliana Shonza amesema kutoshirikishwa kwa wabunge wa viti maalum katika kamati za fedha za halmashauri kumewafanya kushindwa kusimamia mikopo ya asilimia nne inayotolewa kwa wanawake.

Shonza ameyasema hayo leo Jumanne Aprili 19, 2022 wakati akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) kwa mwaka 2022/2023.

Amesema wanawake wamewaamini kwenda kusimamia maslahi yao lakini katika vikao hivyo ambavyo vinajadili masuala yote ya fedha wabunge hao wamekuwa hawaingii.

“Fedha zinatolewa lakini hazirejeshwi sisi ambao tunakaa na hao watu tunajua changamoto zao, hatushirikishwi katika vikao vya kamati za fedha,”amesema.

Hata hivyo, Spika wa Bunge, Dk Tulia Akson amesema hoja hiyo imekuwa ikija na kuondoka lakini anafiriki ni muhimu kwa wabunge wanawake kukutana na kuwekana sawa kuhusu jambo hilo.

Amesema mbunge wa viti maalum anawakilisha halmashauri zote za mkoa wake na hawezi kuwa mjumbe wa kamati za fedha za halmashauri zote.

Advertisement “Ndio maana nasema lazima tukalizungumze kwa sababu wabunge wa majimbo wapo na wa viti maalum wapo tunaweza kushauriana vizuri kuhusu jambo hili, kuliko kufikiri ni jambo rahisi, ” alisema.

Dk Tulia amesema ndio maana jambo hilo linajitokeza kila bajeti ya Tamisemi na halipati majibu kwa sababu kuna changamoto ambazo zinatakiwa kuzungumzwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live