Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shinini Mwenyekiti mpya UWT

DB70EE53 8829 4495 82EE D4B1283CF2DC.jpeg Shinini Mwenyekiti mpya UWT

Sun, 16 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wajumbe wa Mkutano mkuu wa Jumuiya ya umoja wa wanawake wa CCM Tanzania (UWT) Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, wamemchagua Anna Shinini kuwa Mwenyekiti wa UWT wa Wilaya hiyo.

Uchaguzi huo umefanyika mji mdogo wa Orkesumet jana Jumamosi Oktoba 15 baada ya kurudiwa.

Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Sezaria Makota ambaye ndiye msimamizi wa uchaguzi huo amemtangaza Shinini kushinda nafasi hiyo kwa kura 137.

Makota amesema wapiga kura walikuwa 223 ila kura mbili zimeharibika na kura halali zilikuwa 130.

Amesema wagombea walikuwa wawili ambapo Agnes Brown amepata kura 84 na Shinini kura 137. "Kwa mamlaka niliyopewa ninamtangaza Shinini kuwa Mwenyekiti wa UWT wa wilaya ya Simanjiro," amesema Makota.

Uchaguzi huo unatarajiwa kurudiwa mara baada ya mmoja kati ya wagombea wa nafasi hiyo kukata rufaa CCM Taifa.

Awali, uchaguzi wa UWT wilaya ya Simanjiro ulifanyika Septemba 24 mwaka huu ambapo kwa nafasi hiyo ya Mwenyekiti ililazimika kurudiwa mara mbili. Katika uchaguzi huo matokeo yalikuwa Anna Shinini aliongoza kwa kupata kura 97, Agnes Brown 86, Naomi Edward 10 na Rehema Yohana 2.

Hata hivyo, ikabidi uchaguzi huo urudiwe tena kutokana na mshindi kutokupata zaidi ya asilimia 50 na matokeo yakawa Agnes kura 99 na Anna kura 96.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live