Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shigongo: Tusiwe na Wasiwasi, Mama Samia yuko Vizuri

Shigongo 1.jpeg?fit=1024%2C683&ssl=1 Shigongo: Tusiwe na Wasiwasi, Mama Samia yuko Vizuri

Tue, 20 Apr 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

Mbunge wa Buchosa, Eric Shigongo amewaasa Watanzania kutokuwa na hofu kwani Rais tuliye naye sasa Mama Samia Suluhu ataendeleza yale mema yote yaliyokuwa yakifanywa na Hayati Dkt. John Magufuli sababu wote walikuwa pamoja, waliahidi pamoja katika Ilani ya uchaguzi ya CCM kuyatekeleza.

Shigongo ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Global Group, amesema hayo leo Jumatatu, Aprili 19, 2021, wakati akifanya mahojiano maalum na Global Radio na Global TV Online.

“Hayati Dkt. Magufuli alitamani kuwapa Watanzania tahamani ya kujivunia kuitwa Watanzania popote walipo Ulimwenguni. Ametoa mchango mkubwa sana kwa nchi yake ambao hauwezi kufutika hata kama tungefanyaje.

“Ukiniambia nimzungumzie Dkt. Magufuli namzungumzia Mzalendo wa Taifa letu, mtu aliyependa watu wake, mwenye uthubutu, alijitoa sadaka maisha yake akijua pengine anaopambana nao (Mabeberu) wana pesa nyingi wangemfanya chochote, lakini hakuogopa.

“Dkt. Magufuli amepumzika, kitabu alichokiandika kwa miaka 61 kitaendelea kusomwa maisha yote mpaka mwisho wa ulimwengu kutokana na mambo makubwa ambayo amelifanyia Taifa letu.

“Tumepata Rais mzuri, mimi kama Shigongo ninalo jukumu la kutimiza wajibu wangu kama mbunge lakini pia kama mwananchi wa kawaida. Tusikae tu na kusema Rais atafanya, Watanzania wote tunao wajibu wa kuwa wazalendo na kulisukuma Taifa letu mbele.

“Mambo yote aliyoyaanzisha Hayati Magufuli yatatekelezwa na Mama Samia, sababu Ilani ya CCM ipo na kinachotekelezwa ni Ilani ya CCM. Hawa wote walikuwa timu moja na lengo lao lilikuwa moja, hakuna kilichobadilika. Mama yupo.

“Watanzania acheni wasiwasi, Mama Samia yupo, ahadi zote zilizotolewa na Magufuli alizitoa pia Mama Samia sababu walikuwa pamoja. Barabara yetu ya Buchosa itajengwa, imeshatengewa fedha na tenda imetangazwa, itaanza kujengwa, iko siku Buchosa utaingia kwa lami.

“Hayati Magufuli alikuwa na sauti kali na vitendo vilionekana, kila jambo lina uzito wake, Mama Samia anaweza kuwa na lugha laini lakini vitendo vyake vikawa vikubwa. Sio sawa kulinganisha uongozi, tumwamini na kumuunga mkono Mama ili mambo yaweze kutimia,” amesema Shigongo.

Chanzo: globalpublishers.co.tz