Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sheria kuvibana vyama vya siasa yaja

Vyama Vya Siasa Siasa Sheria kuvibana vyama vya siasa kujumuisha wanawake kwenye uongozi yaja

Wed, 1 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imesema itapeleka bungeni marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa ili kuvilazimisha kuwa na sera itakayoweka mwongozo wa kujumuisha wanawake katika kuwania nafasi mbalimbali za uongozi.

Naibu Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, Ummy Ndeliananga leo Jumatano Novemba Mosi, 2022, Mbunge wa Vitimaalum Anatropia Theonest.

Anatropia amesema kulingana na takwimu zilizotolewa na Serikali ni wastani wa wanawake 24 hushinda ubunge katika uchaguzi mkuu kila baada ya miaka mitano.

Amesema wanawake hao ni wachache sana kuwakilisha katika nafasi ya ubunge licha ya Serikali kuridhia mikataba mbalimbali ya kimataifa ya kuongeza ushiriki wa wanawake.

“Ni mkakati gani mahususi unaopaswa kufanyiwa mapitio ili kuongeza idadi ya ushiriki wa wanawake katika siasa,” amehoji.

Pia ametaka kufahamu ni mkakati gani wa serikali kubadilisha Sheria ya Uchaguzi ili kuvilazimisha vyama vya siasa kuwa na idadi maalum ya wanawake kwenye chaguzi mbalimbali nchini.

Akijibu swali hilo Ummy amesema Serikali inatambua umuhimu wa wanawake kushiriki katika vyama vya siasa.

Amesema mkakati uliopo ndani ya ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kuendelea kutoa elimu kwa makundi ya wanawake waweze kujiamini na kujiandaa kugombea nafasi hizo.

“Lakini tutaleta mabadiliko bungeni ya Sheria ya Vyama vya Siasa ili kuvitaka vyama vya siasa kuwa na sera ambazo zitaweka mwongozo mahususi wa kujumuisha wanawake katika kugombea nafasi mbalimbali,” amesema.

Katika swali la msingi Anatropia amehoji ni wanawake wangapi wamekuwa wabunge wa majimbo na madiwani katika chaguzi tatu mfululizo zilizopita.

Akijibu swali hilo, Ummy amesema katika kipindi cha kuanzia 2010 hadi 2020 zilifanyika chaguzi tatu katika ngazi ya ubunge na udiwani jumla ya wanawake 73 walishinda na kuchaguliwa kuwa wabunge wa majimbo.

“Kwa upande wa madiwani jumla ya wanawake 654 waliweza kuchaguliwa na hivyo kuwa madiwani katika Kata husika,” amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live