Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shehe Ponda kukutana na kamati maalum ya Rais Samia

Sheikh Pondaa Shehe Ponda

Sun, 8 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi kazi kilichoundwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuhusu masuala ya demokrasia ya vyama vingi vya siasa nchini kitaanza awamu ya tatu ya kupokea maoni kwa siku tisa na katika awamu hii wadau wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa watatoa maoni yao.

Taarifa iliyotolewa Dodoma na Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa kupitia kwa Katibu wa Kikosi kazi hicho, Sisty Nyahoza ilisema wadau hao watatoa maoni yao kwa siku tisa kuanzia Mei 10, mwaka huu katika Ukumbi wa Adam Sapi Mkwawa katika Ofisi ndogo za Bunge, Dar es Salaam.

Wadau hao ni pamoja na jumuiya za wanafunzi wa elimu ya juu, Ismail Jusa, Profesa Issa Shivji, Dk Hellen Kijo Bisimba, Askofu Benson Boganza, Shehe Ponda Issa Ponda, Jumuiya ya Wahindu na wengine

Chanzo: www.tanzaniaweb.live