Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shaka ateta na viongozi DWJ

Shaka Dwj Shaka ateta na viongozi DWJ

Fri, 30 Sep 2022 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Viongozi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Mkoa wa Dodoma (DWJ) wametembelea ofisi za Makao makuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa lengo la kujitambulisha, kueleza kazi wanazozifanya na kuomba ushirikiano.

Viongozi hao  walitembelea  ofisi hizo Septemba, 28, 2022 na kukutana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka aliyewapongeza kwa kuwa na umoja na kufanya kazi za kurejesha kwa jamii.

"Nawapongeza kwa kujiunga katika umoja wenu pamoja na kazi mnazozifanya za kugusa maisha ya jamii hususani watu walio katika mazingira magumu kama mayatima, wagonjwa, wahitaji wengine na uhifadhi wa mazingira.

“Nawahakikishia CCM tutawaunga mkono. Ombi langu kwenu pamoja na kazi nzuri ya uandishi wa habari mnayoifanya nawaomba andikeni kazi kubwa na nzuri inayofanywa na serikali ya awamu ya sita ili jamii ijue nini serikali yao inafanya na kuwanyima fursa wapotoshaji kupata himaya kwenye jamii yetu." alisema Shaka

Shaka alitoa rai kwa viongozi hao kwa kuwataka kutumia kalamu na taaluma zao kueleza mafanikio ya utendaji wa serikali na kuwasaidia watanzania kwa kuibua changamoto mbalimbali wanazopitia.

Kwa sasa DWJ inawahudumia wanafunzi watano wa kidato cha 5 na sita, inahudumia mwanamke mmoja mtu mzima mwenye tatizo la mifupa aliyelazwa taasisi ya mifupa Muhimbili (MOI) na wanatekeleza programu ya upandaji miti jiji la Dodoma.

Advertisement

Chanzo: www.mwananchi.co.tz