Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shaka ashauriwa kusoma machapisho

Wasiraaa.jpeg Shaka ashauriwa kusoma machapisho

Tue, 25 May 2021 Chanzo: ippmedia.com

Wasira alitoa ushauri huo  leo jijini Dar es Salaam wakati alipokutana na Shaka katika ofisi ndogo ya Makao Makuu ya CCM lumumba  jijini Dar es Salaam.

Viongozi hao wamezungumza kwa kina masuala mbalimbali yanayohusu Itikadi na Uenezi kwa kuwa idara yake ndio kikosi kinachotakiwa kwenda katika vita kwa ajili ya mapambano.

Alisema mantiki ya idara hiyo si kuwa msemaji peke yake wa chama bali  ni idara nyeti inayomhitaji mwanasiasa anayetosha kuizumgumzia, kuielezea na kuifafanua siasa, sera na itikadi ya chama.

Alisema ameupongeza uamuzi wa Mwenyekiti  wa CCM, Rais Samia Suluhu Hassan kumteua Katibu Mkuu mpya kijana anayetokana na CCM, Daniel Chongolo na kumteua Shaka.

Wasira alisema kuwa wajumbe wengine wa sekreterieti wanatosha kwani miongoni mwao wapo wazoefu, viongozi mahiri na wengine mashuhuri waliowahi kuhimili  purukushani na mikiki ya kisiasa.

"Umefanya kazi nzuri sana ukiwa Naibu Katibu Mkuu UVCCM Zanzibar na baadae Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa. Ulichapakazi ya kijasiri ukijibu mapigo ya upinzani kwa wakati na kwa nguvu ya hoja," alisema Wasira.

Kwa upande wake,  Shaka alisema atakwenda kuufanyia kazi ushauri wa Wasira kupokea ushauri  pamoja na kumpa moyo katika juhudi za kutimiza wajibu wake na kupigania maslahi mapana ya CCM.

Shaka alisema yote  ambayo amekuwa akiyajibu, kuyasema na kutetea chama huwa si maneno yanayotoka moja kwa moja mdomoni mwake bali huwa tayari ameyadurusu kitambo toka kwenye vitabu vya kumbukumbu muhimu za kisiasa, sera, dira na kujua chama kilipotoka, kilipo na kinakotaka kuelekea.

Alisema wanasiasa mahiri na mashuhuri duniani wamejifunza, kuelekezwa hatimaye wakafahamu na kuelewa kutoka  kwa wanasiasa waliowatangulia kwani hata walimu nao wana wakufunzi wao.

Chanzo: ippmedia.com