Katie wa Itikadi na Uuenezi Shaka pia ametamka Mbatia kuelezea mikakati ya chama chake ili kuwavutia wananchi kujiunga na chama hicho kukubali na kusifu kusifu hatua zinazochukuliwa na Serikali ya awamu sita .
Ameeleza hayo Januari 2, 2021 wakati akijibu madai mbalimbali ya Mbatia ambaye mapema jana alikutana na wanahabari na kuzungumza masuala mbalimbali ikiwemo kuwataka wananchi kutomshambulia Spika wa Bunge, Job Ndugai kutokana na msimamo wake kuhusu Serikali kukopa.
SOMA: Mbatia ataka Ndugai asishambuliwe
Katika maelezo yake na wanahabari, Mbatia alisema kutofautiana kuhusu suala la kukopa kati ya Rais Samia Suluhu Hassan na Ndugai mjadala wao unaleta afya kwa sababu mihimili ya Bunge na Serikali inapokinzana ndio afya katika Taifa.
Mbatia alikwenda mbali zaidi na kutaka Ndugai asishambuliwe wala kutukanwa kutokana na msimamo wake kuhusu kukopa huku akiwataka watu kujadili hoja yake kwa mtazamo chanya na sio kumshambulia Ndugai binafsi.
Lakini Shaka amemtaka Mbatia kukinusuru chama chake ili kiwe chenye nguvu kitakachojadili nguvu ya hoja.
Amesema kupatia kutamka takwimu au kukosea hakuwezi kumsaidia mwananchi wa kawaida anayeishi vijijini.
Kuhusu suala la takwimu, Mbatia alisema itumike busara kwa Serikali kuomba radhi kuhusu takwimu zilizotangazwa na Rais Samia wakati akitoa salamu za kufunga na kuufungua mwaka mpya.
"Anapoonekana kiongozi kama Mbatia aking'angania jambo lisilo na msingi wowote ni fedheha kwake na kwa chama chake.Wananchi wasomi na wenye maarifa wamekuwa wakiisifu utawala wa Rais Samia yakiwemo mataifa makubwa na taasisi za kimataifa.
Lakini Shaka amesema, "Kukosea kutaja takwimu au kupatia si hoja yenye maana na mashiko. Mbatia atazame kwanza utendaji wa Serikali jinsi unavyotekeleza majukumu ya kisera yanayoleta manufaa kwa jamii," amesema Shaka.
Shaka amesema kutamka takwimu kwa kupatia au kukosea haliwezi kugeuzwa ndio mjadala wenye maana kwani kupatia au kukosea ni masuala ya kawaida na yasiyoweza kuzuilika kibinadamu