Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shaka afanya mazungumzo na Wasira "ulijibu mapigo ya upinzani"

WhatsApp Image 2021 05 25 At 17.58.48 660x400.jpeg Shaka afanya mazungumzo na Wasira "ulijibu mapigo ya upinzani"

Wed, 26 May 2021 Chanzo: millardayo.com

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka ametembelewa na kufanya mazungumzo na Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM ya Taifa Ndg Steven Masato Wasira katika ofisi ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba jijini Dar es salaam.

“Umefanya kazi nzuri sana ukiwa Naibu Katibu Mkuu UVCCM Zanzibar na baadae Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa, ulichapakazi ya kijasiri, ukijibu mapigo ya upinzani kwa wakati na kwa nguvu ya hoja. Umekuwa ukipangua  hoja kwa mirejesho ya kisiasa, kihistoria aidha ya TANU au ya ASP endelea hatuna hofu nawe kwenye nafasi hii” Mzee Masato Wasira (MNEC)

” Siku zote wanasiasa mahiri na mashuhuri sana duniani wamejifunza, kuelekezwa, kuandaliwa, kukoselewa na kushauriwa lakini hatimaye hufahamu na kuwa mweledi hasa ukikubali kujifunza toka kwa wanasiasa waliokutangulia kwani hata walimu nao wana wakufunzi wao, kwa uwezo MwenyeziMungu sitawangusha” Shaka Hamdu Shaka. Katibu NEC Itikadi na Uenezi



“SERIKALI IONYESHE MAKALI” MWANYIKA AKIPIGANIA ZAO LA CHAI BUNGENI
Chanzo: millardayo.com