Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shaka: Rais Samia amefungua fursa za uchumi

Shakaakakakakaka Shaka Hamdu Shaka, Katibu Itikadi na Uenezi CCM

Mon, 4 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapindiuzi (CCM) Taifa Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka amesema ndani ya kipindi cha mwaka mmoja katika uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan kazi kubwa imefanyika katika diplomasia ya uchumi, katika kufungua fursa za kiuchumi.

Shaka amesema hayo leo Jumatatu Julai 4, 2022 katika kipindi cha ‘Good Morning’ cha Wasafi Media, wakati wa ziara yake ya kutembelea vyombo vya habari.

 “Rais Samia alipoingia madarakani alisema mpeni nafasi aifungue nchi, na tunaona amefungua fursa mbalimbali na kuipeleka Tanzania duniani” amesema.

Amesema Rais Samia kwenye nyanja za uchumi na uwekezaji mradi wa Lindi na Mtwara ndio mradi mkubwa katika uongozi wake.

“Mradi wa Gesi asilia LNG (Liquefied Natural Gas), unakwenda kugharimu dola za Kimarekani trillion 30, sawa na zaidi ya Sh70 trilioni ya fedha za Kitanzania” amesema

Ameeleza kuwa mradi huo wa Lindi na Mtwara unakwenda kushusha maisha ya Watanzania na pia utaleta ushindani wa kuonyesha ni kwa namna gani biashara hizi zinakwenda kufungua njia ya kuwatoa Watanzania katika dimbwi la umaskini, hivyo wananchi wategemee mabadiliko makubwa.

Shaka amesema kuhusu Suala la Katiba mpya, kwa CCM sio hoja mpya kwani mwaka 2011 walishaibeba hoja hiyo ya msingi ya kupatikana kwa katiba mpya.

“Itapatikana Katiba mpya ambayo inatokana na historia ya nchi hii” amesema Shaka.

Amesema ziara yake katika vyombo mbalimbali vya habari ni kutengeneza mahusiano mazuri kati ya vyombo hivyo na CCM.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live