Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shabiby ashangaa kushamiri kwa maudhui ya kichawi, kiganga

Mbunge Wa Cairo Shabiby Shabiby ashangaa kushamiri kwa maudhui ya kichawi, kiganga

Fri, 24 May 2024 Chanzo: dar24

Mbunge wa Jimbo la Gairo, Ahmed Shabiby ameiomba bodi ya Filamu Nchini kupitia Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kurusha mahudhui yanayofaa kwenye vituo vya Luninga, kwani kuna mapungufu na maudhui ya kichawi na kiganga yameshamiri.

Akizungumza Bungeni Jijini Dodoma wakati akichangia bajeti ya Wizara hiyo, Shabiby amesema Wizara na Bodi ya filamu wanatakiwa kuzingatia  jambo hilo kwani filamu ambazo zinatisha watu hazijengi wala kufundisha bali zinawaharibu waaribu watu kisaikolojia.

“Na sio watu wazima tu hata watoto wadogo wanaharibika kutokana na filamu hizo za kutisha, ni mnawaandaa watoto kuwa waganga wa kienyeji wa badaae kutokana na filamu zenu zisizofaa, ndiyo maana Watanzania wengi wanashinda mitandaoni kufuatilia umbea tu maana hata wakienda kutanzama televisheni hamna cha maana,” amesema Shabiby.

Chanzo: dar24