Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sh3.4 milioni zatumika kumtunza Faru Fausta kwa mwaka

16745 Pic+faru TanzaniaWeb

Tue, 11 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Serikali inatumia Sh3.4 milioni kwa mwaka kwa ajili ya matunzo ya Faru Fausta (54) aliyehifadhiwa hifadhi ya Ngorongoro, bunge limeelezwa leo septemba 11, 2018.

Serikali imeeleza leo kuwa gharama za kumtunza mnyama huyo kwa sasa zimeshuka kutoka Sh1. 4 milioni kwa mwezi ambayo kwa mwaka ingekuwa ni Sh17.34 milioni.

 Kwa sasa matunzo ya Faru huyo ni Sh285, 000 kwa mwezi.

Akizungumza leo Septemba 11 bungeni, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Japhet Hasunga amesema uamuzi wa kumtunza Faru huyo ulitokana  na uamuzi wa kunusuru maisha yake ili aendelee kuwa kivutio cha utalii na kuingiza fedha za kigeni nchini.

Katika swali la msingi Mbunge wa viti Maalumu Suzan Lymo (Chadema) amehoji ni kipi kilicho muhinu kati ya kumtunza Faru Fausta au Wazee ambao hawana walezi.

Waziri Nditiye amesema Faru huyo ambaye alizaliwa 1965 alijeruhiwa na fisi hivyo lazima atunzwe ili kumnusuru.

Kuhusu wazee amesema serikali imeweka sera nzuri za kuwatunza. Hata hivyo wabunge walipiga kelele zaidi wakipinga kuhusu majibu hayo.

Chanzo: mwananchi.co.tz