Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yawaweka kiporo kina Mbatia

SIMBACHAWENE WEB.jpeg Serikali yawaweka kiporo kina Mbatia

Sun, 31 Jul 2022 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, George Simbachawene amejitosa kwenye mgogoro wa chama cha NCCR-Mageuzi, ikiwa ni siku chache tangu Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi kutangaza kujitoa kama msuluhishi.

Hatua hiyo imekuja baada ya mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi aliyesimamishwa, James Mbatia kumwandikia barua Simbachawene akimtaka asaidie kutatua mgogoro ndani ya chama chake.

Julai 18, Jaji Mutungi alitangaza kujitoa kwenye mgogoro huo kwa kile alichoeleza ni kuheshimu katiba ya NCCR-Mageuzi, lakini pia uamuzi wa Mbatia kulifikisha jambo hilo kwa Waziri Simbachawene.

Akizungumza jana jijini hapa, Waziri Simbachawene alieleza kwa kifupi suala hilo atalitolea ufafanuzi wiki ijayo.

“Hilo nitalizungumzia wiki ijayo. Nipigie simu wiki ijayo,” alisema waziri huyo wakati akitoka kuzungumza na waandishi wa habari kuhusu mkakati wa utekelezaji wa bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2022/23.

Mgogoro huo ulipamba moto Mei 21, mwaka huu baada ya halmashauri kuu ya NCCR Mageuzi kumsimamisha Mbatia na makamu mwenyekiti (Bara), Angelina Mtahiwa kujihusisha na shughuli zozote za chama hadi watakapoitwa kwenye mkutano mkuu wajieleze kuhusu tuhuma zinazowakabili.

Hata hivyo, Mbatia na wafuasi wake walipinga uamuzi huo wakisema kikao hicho kilikuwa batili. Waliituhumu Ofisi ya Msajili kuchochea mgogoro huo, hasa baada ya Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza kuhudhuria mkutano huo.

Msajili aliwaita viongozi wa pande mbili zinazokinzana kwa lengo la kuzungumza, lakini upande wa Mbatia pekee ndio walihudhuria kikao hicho.

Chanzo: www.mwananchi.co.tz