Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yawasilisha mapingamizi matatu dhidi ya Nassari

49011 Nasaripic

Wed, 27 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma imepanga kutolea uamuzi wa mapingamizi matatu ambayo yamewekwa na upande wa Serikali katika kesi ya maombi madogo ya kufungua kesi msingi kwa ajili ya kutengua uamuzi wa Spika wa Bunge wa kumfutia ubunge aliyekuwa Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari.

Maombi hayo yalifunguliwa Machi 29 mwaka huu. Jaji Latifa Mansoor anayesikiliza kesi hiyo namba 22 ya mwaka 2019 ameahirisha kesi hiyo leo hadi Machi 29 mwaka huu kwa ajili ya kusikiliza mapingamizi hayo ambayo hata hivyo hayakutajwa mahakamani hapo.

Maamuzi hayo yanakuja baada Mahakama kupokea mapingamizi yaliyowasilishwa na upande wa Serikali ukiwakilishwa na mawakili wawili ambao ni Alisia Mbuya na Masunga Kawahanda.

Machi 20 mwaka 2019 mahakama ilitoa siku saba kwa upande wa Serikali kupeleka kiapo kinzani cha maombi hayo.

Jaji aliagiza pia kusifanyike uchaguzi wowote jimboni hadi hapo maombi hayo yatakaposikilizwa na kutolewa uamuzi.

Nassari ambaye alikuwepo mahakamani hapo amewakilishwa na mawakili wawili Hekima Mwasipe na Fred Kalonga.

Related Content

Hata hivyo Jaji ameieleza mahakama kuwa shauri hilo litasikilizwa tena Machi 29, 2019 kwa ajili ya uamuzi wa mapingamizi hayo ya upande wa Serikali.



Chanzo: mwananchi.co.tz