Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yakiri kupata taarifa vurugu za uchaguzi

E58c69be18638e969d00da3bf4e008a7.jpeg Serikali yakiri kupata taarifa vurugu za uchaguzi

Thu, 13 May 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

SERIKALI imekiri kupata taarifa za kutokea kwa vurugu zilizosababishwa na wananchi katika Halmashauri ya Wilaya ya Liwale na kuleta uvunjifu wa amani, uharibifu wa vitu mbalimbali ikiwemo mali za wananchi na serikali wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Patrobas Katambi, aliliambia Bunge jijini Dodoma jana wakati wa akijibu swali la msingi la Mbunge wa Liwale, Mohamed Kuchauka (CCM) kuwa, serikali inakiri kupata taarifa za kutokea kwa vurugu zilizosababishwa na wananchi katika Halmashauri ya Wilaya ya Liwale.

Katika swali lake, Kuchauka alisema: "Wakazi wa Liwale waliathirika na vurugu za uchaguzi wa mwaka 2020; na mali za wananchi na serikali zilichomwa moto” hivyo, akataka kujua mpango wa serikali kuwafuta machozi wananchi kupitia Mfuko wa Maafa.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri Katambi alisema: "Uhalifu huo umefanyika wakati wa Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 28, 2020 katika Jimbo la Liwale na maeneo mengine mkoani Lindi. Aidha, serikali ilifanya jitihada mbalimbali za kumaliza vurugu hizo kwa kutumia vyombo vya ulinzi na usalama.

"Kwa mujibu wa sheria za nchi yetu, kufanya vurugu za aina hii ni kosa la jinai. Hivyo, matokeo ya madhara ya vurugu hizo yatashughulikiwa kwa mujibu wa sheria zinazohusu masuala ya makosa ya jinai.

Alisema Sheria ya Menejimenti ya Maafa ya Mwaka 2015 na kanuni zake za utekelezaji hazina ufungamanisho wa pamoja na madai ya kijinai na hasa yahusuyo uharibifu wa mali na namna ya kulipa fidia.

"Napenda kuwapa pole wale wote walioathirika na vurugu hizo na kuwaomba wananchi kuzingatia sheria, kanuni na taratibu ili kudumisha amani na usalama nchini," alisema.

Chanzo: www.habarileo.co.tz