Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali ya UPDP kutoa matibabu bure

725ba9281b8db46d0a279ec7ea483b46.png Serikali ya UPDP kutoa matibabu bure

Tue, 20 Oct 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MGOMBEA urais kupitia Chama cha UPDP, Twalib Kadege amesema akichaguliwa, atahakikisha kila Mtanzania anapata tiba bure, kwa kuwa ni haki ya kila mwananchi.

Alitoa ahadi hiyo kwenye mkutano wa kampeni katika viwanja vya Soko la Gungu Kwa Zulu Natal Manispaa ya Kigoma Ujiji.

Aliomba wananchi wamchague na pia wawachague wagombea wengine wa chama hicho, kwa kuwa suala la tiba ni miongoni mwa mambo muhimu kwenye jamii.

Kadege alisema serikali inapaswa kuimarisha ukusanyaji kodi kutoka vyanzo mbalimbali ili kugharamia huduma muhimu za kijamii zikiwemo huduma za tiba, badala ya kuwatoza fedha nyingi watu mahututi kitandani ambao hawana uwezo wa kufanya kazi.

Alisema, Tanzania ina rasilimali nyingi yakiwemo madini na hifadhi za taifa, hivyo serikali inapaswa kukusanya fedha kutoka kwenye vyanzo hizo ili itekeleze sera ya huduma bure za matibabu.

Mgombea huyo pia alisema kilimo ni msingi mwingine wa sera za chama hicho na atakapoingia madarakani, chama chake kitaboresha sekta ya kilimo kwa kuondoa jembe la mkono ili wananchi walime kisasa.

Kadege alisema kilimo kikiimarishwa, kitakuwa kimbilio la watu wengi hivyo kupunguza kasi ya wananchi kukimbilia mijini, kwa kuwa wataona umuhimu wa kubaki vijijini walime kibiashara.

Mgombea ubunge wa Jimbo la Kigoma Mjini kupitia chama hicho, Mchungaji Michael Cyprian alisema jimbo hilo linahitaji watu wenye dhamira ya kweli ya kuwatumikia Watanzania kama ambavyo UPDP kupitia viongozi wake imeonesha vipaumbele, ambavyo vikitumika vizuri vina uwezo wa kuwakomboa kiuchumi Watanzania.

Chanzo: habarileo.co.tz