Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali ya Tanzania yashinda rufaa ya Ma DED kusimamia uchaguzi

80410 Pic+ded

Thu, 17 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mahakama ya Rufani nchini Tanzania imetengua hukumu na amri ya Mahakama Kuu ya kuzuia wakurugenzi wa halmashauri, manispaa na majiji kusimamia Uchaguzi Mkuu kwa niaba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

SOMA ZAIDI: Serikali kuikatia rufaa hukumu ya wakurugenzi kusimamia uchaguzi

Uamuzi huo umetolewa leo Jumatano Oktoba 16, 2019 na Mahakama hiyo. Kwa maana hiyo wakurugenzi wanaruhusiwa kusimamia uchaguzi.

Serikali ya Tanzania iliamua kukata rufaa kupinga hukumu ya Mahakama Kuu kuwazuia Wakurugenzi hao kusimamia uchaguzi.

SOMA ZAIDI: NEC: Tutafuata uamuzi wa mahakama uchaguzi mkuu

Uamuzi huo ulitokana na Mahakama Kuu katika hukumu yake iliyotolewa na jopo la majaji watatu, Dk Atuganile Ngwala, Dk Benhajj Masoud na Firmin Matogolo ilibatilisha kifungu cha 7(1) cha Sheria ya Uchaguzi kinachoipa mamlaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuwateua wakurugenzi wa majiji, manispaa na miji kuwa wasimamizi wa uchaguzi.

Pia Soma

Advertisement

Pia ilibatilisha kifungu cha 7(3) kinachoipa NEC mamlaka ya kuteua mtu yeyote miongoni mwa watumishi wa umma kuwa msimamizi wa uchaguzi.

SOMA ZAIDI: Lissu asema Katiba inakiukwa wakurugenzi kusimamia uchaguzi

Katika hukumu hiyo mahakama hiyo ilisema kwamba vifungu hivyo ni kinyume cha Katiba ya nchi ikibainisha kuwa wakurugenzi hao huteuliwa na Rais aliyeko madarakani ambaye hutokana na chama tawala na kwamba wengine ni wanachama wa chama cha mamlaka inayowateua jambo ambalo huathiri utendaji wao katika kutenda haki.

Pia ilisema kwamba sheria haijaweka ulinzi kwa NEC kumteua mtumishi yeyote wa umma kuhakikisha kuwa anakuwa huru katika kutekeleza majukumu yake.

SOMA ZAIDI: Mahakama yapiga 'stop' wakurugenzi kusimamia uchaguzi

Uamuzi huo wa Mahakama Kuu umetokana na kesi iliyofunguliwa na mashirika kadhaa ya wanaharakati kupitia kwa mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Bob Wangwe, akitetewa na Wakili Fatma Karume.

Mahakama Kuu imesikiliza maombi ya ACT- Wazalendo kujiunga katika kesi ya ukomo wa urais. Uamuzi wa ama wataruhusiwa au la utatolewa Oktoba 24, 2019.

SOMA ZAIDI: Mahakama yafuta wakurugenzi kusimamia uchaguzi Tanzania

Chanzo: mwananchi.co.tz