Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali ya Rais Kabila wa DRC iko hatarini kupinduliwa?

1607 S4.reutersmedia.net  660x400 TZW

Mon, 22 Jan 2018 Chanzo: millardayo.com

Leo January 19, 2018 Taarifa kutokea nchini DRC Congo jioni ya leo ni kutanda kwa hofu na wasiwasi kwa wananchi wa Mjini Kinshasa baada ya Jeshi kuizunguka Ikulu ya Rais Joseph Kabila.

Asubuhi ya leo January 19, 2018 Waandishi wa Habari nchini DRC Congo wamesema Kamanda mmoja wa cheo cha Jenerali aitwaye John Tshibangu alitangaza kuasi na kumpa Rais Kabila siku 45 awe amejiuzulu.

Kamanda huyo alitangaza hilo kupitia mkanda wa video ambayo ilisambaa kupitia mitandao ya kijamii ambapo Kamanda huyo alimwambia Rais Kabila kuwa ana siri yake na hivyo ataitoa kama hataondoka madarakani.

Pia amemweleza kuwa ni lazima aombe msamaha kwa raia wa Congo kwa kosa la kushindwa kuiongoza nchi.

Chanzo: millardayo.com