Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali ya CCM kuboresha huduma za afya

0 Serikali ya CCM kuboresha huduma za afya

Thu, 10 Sep 2020 Chanzo: dar24.com

Mgombea mwenza kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM ) Samia Hassani amesema kuwa CCM itaendelea kuboresha huduma za afya kwenye maeneo yote nchini.kwa kujenga miondombinu ,vifaa tiba na kuongeza watumishi .

Mwarobaini wa kusaidia wakulima na walaji huu hapaAkihutubia wananchi waliojitokeza kusikikiliza kampeni za chama hicho , Halmashari ya mji Nanyamba mkoani Mtwara , mama Samia amesema kuwa serikali itasisitiza matumizi ya bima ya afya ili kutoa huduma hiyo bila malipo ikiwa ni moja ya njia ya kuzuia vifo vya mama wajawazito na watoto wenye umri chini ya miaka mitano .

“serikali itatongeza vituo vya kutolea huduma ya afya vingi kama inavyowezekana ,kama ilani yetu ilivyosema kujenga  vituo vya afya kila katawahidi kwamba tutaendelea kujenga vituo vya afya katika kata zisizo navyo,” amesema Samia .

Maalim Seif atakavyopambana na wanaompingaAidha mama Samia amesema kuwa serikali inajipanga kujenga hospitali katika halmashauri 98 kwa yale maeneo ambayo hazijapa hospitali hizo .

Mgombea huyo wa CCM anaendelea na kampeni mkoani Mtwara ikiwa nikutafuta ushindi kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba.

Chanzo: dar24.com