Chama cha ACT Wazalendo kimeitaka Serikali kupunguza mzigo wa gharama za maisha kwa Wananchi kwa kusitisha Nauli Mpya za Daladala na Mabasi zilizoanza kutumika Desemba 2023 pamoja na kushusha Bei ya Sukari inayolalamikiwa Nchi nzima
Chama cha ACT Wazalendo kimeitaka Serikali kupunguza mzigo wa gharama za maisha kwa Wananchi kwa kusitisha Nauli Mpya za Daladala na Mabasi zilizoanza kutumika Desemba 2023 pamoja na kushusha Bei ya Sukari inayolalamikiwa Nchi nzima Kupitia taarifa yake, #ACTWazalendo imesema kitendo cha Serikali kuridhia maamuzi ya #LATRA inaonesha wazi haiwajali Wananchi kwasababu nauli zimeangalia maslahi ya Wasafirishaji na si hali za Wananchi wa kawaida - Pia, imeitaka Serikali kufanyia kazi madai ya Wasafirishaji kwa kurejesha ruzuku kwenye Mafuta pamoja na kuhimiza matumizi ya Gesi Asilia kwenye Vyombo vya Usafirishaji ili kupunguza gharama zinazotokana na Mafuta - Aidha, kuhusu Sukari, Chama hicho kimesema Serikali ichukue hatua za haraka kuhakikisha Sukari inapatikana ili Wananchi wauziwe kwa Bei nafuu kwasababu hadi sasa kauli za Serikali hazijasaidia chochote.