Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sendiga ataka viongozi wasijilipe posho

Sendiga Web Sendiga ataka viongozi wasijilipe posho

Fri, 4 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa mkoa wa Rukwa Queen Sendiga, ametoa wito kwa wafanyakazi pamoja na viongozi wengine wanapokwenda kukagua miradi ya maendeleo kuhakikisha hawajilipi posho kutoka katika fedha za miradi husika ili fedha hizo ziweze kukamilisha miradi kwa wakati.

Wito huo umetolewa wakati wa ziara yake ya ukaguzi miradi ya maendeleo wilayabni Nkasi, Kata ya Kala, Kijiji cha Kingo'mbe ambapo pia kuna ujenzi wa kituo cha afya kinachoghalimu milioni 500 zikiwa ni fedha za tozo.

"Azma ya mafundi wanaotekeleza ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo lengo la ni kuhakikisha wanakamilisha ujenzi kwa wakati hivyo kuomba kupewa maslahi yao kwa wakati na mahitaji ya ujenzi," amesema RC Sendiga

Chanzo: www.tanzaniaweb.live