Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Selasini aituhumu taasisi ya maji kwa ubaguzi

Fri, 5 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Mbunge wa Rombo (Chadema), Joseph Selasini amemuomba Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso kutembelea jimboni kwake kutatua tatizo la taasisi ya maji ya Kili Water kwa madai kuwa inagawa maji kwa upendeleo.

Akiuliza swali bungeni leo, Selasini alisema Serikali inatekeleza mradi wa kutoa maji kutoka ziwa Chala na kupanua mtandao wa maji jimboni humo, lakini taasisi hiyo imekuwa ikigawa huduma hiyo muhimu kwa upendeleo na kwa Serikali imekubali kuiondoa.

“Je, mheshimiwa waziri upo tayari kuja Rombo ili kuhakikisha kuwa taasisi hiyo haigawi maji kwa upendeleo hadi hapo itakapovunjwa?” alihoji.

Akijibu, Aweso alisema maji ni uhai na hivyo hakuna haja ya upendeleo.

“Niko tayari kutembelea Rombo kutatua tatizo hilo ili wananchi waweze kupata maji,” alisema.

Katika swali la msingi, Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Dk Christiane Ishengoma alitaka kufahamu Serikali ina mkakati gani wa makusudi wa kumaliza tatizo la maji katika manispaa Morogoro.

Akijibu, Aweso alisema Serikali kupitia Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Morogoro (Moruwasa) inaendelea na uboreshaji wa huduma hiyo katika manispaa hiyo  kwa mipango ya muda mfupi na mrefu.



Chanzo: mwananchi.co.tz