Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Selasini aikingia kifua Mahakama

Selasini Kubaliano.png Selasini aikingia kifua Mahakama

Tue, 27 Sep 2022 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Makamu Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi-Bara, Joseph Selasini amewataka viongozi wa vyama vya siasa kuanza kuheshimu katiba na demokrasia ndani ya vyama vyao kabla ya kulilia demokrasia ya nchi.

Selasini ameyasema hayo jana Jumatatu, Septemba 26, 2022 jijini Dodoma wakati akimjibu aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho James Mbatia.

Juzi, Mbatia alisema kikao kilichofanyika mwishoni mwa wiki cha kumvua uanachama ni kuingilia uhuru wa Mahakama kwa madai uamuzi huo umefanyika kipindi ambacho kina kesi inayoendelea mahakamani.

“Mahakama ya nchi yetu imefanya kazi vizuri, isichafuliwe na watu ambao wanatafuta madaraka, isichafuliwe na waroho wa madaraka. Katika amri zote mbili hakuna iliyozuia mikutano yetu,” amesema.

Amesema viongozi wa vyama vya upinzani wanakuwa na msuli wa kuzungumzia mafisadi ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Serikali lakini wanakosa misuli ya kuzungumzia mafisadi ndani ya vyama vyao.

Chanzo: www.mwananchi.co.tz