Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sanya amuomba radhi Wasira, wamaliza tofauti zao

34890 Pic+wasira Tanzania Web Photo

Fri, 4 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Musoma. Aliyekuwa Mwenyekiti CCM Mkoa wa Mara,  Chiristopher Sanya amemuomba radhi mbunge wa zamani wa Bunda, Steven Wasira akieleza kuwa mambo yaliyotokea baina yao miaka ya nyuma ni upungufu wa kibinadamu.

Sanya amemuomba radhi Wasira ambaye ni mjumbe wa halmashauri kuu CCM leo Januari 4, 2019 katika ukumbi wa chama hicho tawala Mkoa wa Mara uliopo katika Manispaa ya Musoma.

Amechukua uamuzi huo baada ya kupewa nafasi ya kutoa neno baada ya kurejeshewa uanachama wa chama hicho.

"Adhabu zetu zinatokana na makundi ndani ya chama. Minong'ono  ilisemwa kuwa Wasira na Sanya hawaelewani. Niombe radhi kwa yote yaliyojitokeza,” amesema.

“Leo nafunga mstari rasmi wa majungu. Tusipokee malumbano toka nje, mimi bado mdogo sana nahitaji kukamilisha njozi zangu na ukisikia mtu kasema eti Wasira ujue ni mchonganishi.”

Amesema amewaomba radhi wanachama wote wa CCM aliowakosea kwa makusudi au bahati mbaya ili kwa pamoja waendelee kukijenga chama hicho.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally amesema kabla ya kuzungumza alimpa nafasi Wasira kuzungumza machache.

Katika maelezo yake Wasira alisema kilichosababisha matatizo ni siasa za makundi na si maneno ya hisia ambayo watu wamekuwa wakiyaeneza, kwamba Sanya alivuliwa uanachama kwa sababu alikuwa kiongozi wa makundi ndani ya chama hicho.



Chanzo: mwananchi.co.tz