Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sangabuye kujengewa bweni la wasichana

573b38afc9a36d8d5dba4eb51b906453 Sangabuye kujengewa bweni la wasichana

Thu, 1 Oct 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MGOMBEA ubunge wa jimbo la Ilemela,jijini Mwanza kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM), Dk Angelina Mabula amewahidi wakazi wa kata ya Sangabuye kuwa atawajengea bweni la wasichana katika shule ya sekondari ya Sangabuye iliyopo katika kata hiyo.

Ahadi hiyo,Dk Mabula wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Igalagala. Dk Mabula alisema tayari Serikali ya CCM imetenga milioni 72 kwajili ya ujenzi wa bweni hilo.

Aliahidi pia atawajengea shule ya sekondari wakazi wa Kabusungu na walimu watakuwepo wakutosha.Alisema katika sekta ya Afya,wamefanikiwa kujenga hospitali ya wilaya ya Sangabuye.

Alisema Serikali imetenga bilioni 1/- kwajili ya kuboresha vifaa tiba na milioni 46 kwajili ya kunoresha miundo mbinu katika hospitali hiyo.

Dk Mabula aliahidi atajenga madarasa mawili katika shule ya msingi Bezi na aliahidi kutoa matofali 4000 kwajili ya ujenzi wa zahanati kisiwa cha Bezi. Alisema Serikali imetenga milioni 300/- kwajili ya kuboresha sekta ya Uvuvi pamoja na ufugaji wa Samaki kwa vizimba.

Aliahidi baada ya uchaguzi Halmashauri itawapimia wakazi wa Bezi maeneo yao na watapewa hati kwajili ya kumiliki ardhi zao kihalali.Alisema katika Kata ya Kayenze jumla ya mkopo wa milioni 60 ilitolewa kwajili ya wanawake,vijana na walemavu.

Mgombea udiwani kupitia CCM katika kata ya Sangabuye,Renatus Murunga aliwahidi wakazi wa kata yake atashirikiania na Dk Mabula katika kuhakikisha wanajenga shule ya sekondari nyingine.

Chanzo: habarileo.co.tz