Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Samia awapa ujumbe huu CCM

SAMIA CCM 1.png Samia awapa ujumbe huu CCM

Tue, 6 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chama tawala nchini Tanzania, Chama cha Mapinduzi (CCM), leo Jumatatu, Februari 5, 2024 kinaadhimishwa miaka 47 tangu kuzaliwa kwake Februari 5, 1977, baada ya kuunganishwa vyama vya Tanganyika African National Union (TANU) na Chama cha Afro-Shirazi Party (ASP).

Katika ukurasa zake za kijamii, Mwenyekiti wa CCM, Rais Samia Suluhu Hassan ameitumia kuzungumzia siku akiandika, “Heri ya miaka 47 toka kuanzishwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM). Imekuwa miaka 47 ya mapinduzi makubwa kwa kila Mtanzania kwenye kila kona ya nchi yetu. Tulipo leo, sipo tulipokuwa miaka 47 iliyopita.

“Tumepiga hatua kubwa za kimapinduzi na za kujivunia zenye matunda mazuri katika uchumi wetu, miundombinu yetu, huduma zetu za afya, maji, kilimo, elimu, nishati, utawala bora, uhuru wa watu, haki na maendeleo kwa ujumla.

“Katika miaka hii 47 tumeendelea pia kubaki wamoja, wenye amani na mshikamano, tunu ambazo hazijawa rahisi kupatikana, kutunzwa na kudumu katika maeneo mengi ya bara letu. Maendeleo ni mchakato, ni hatua inayotaka juhudi na weledi wa kila mmoja wetu.

“Tafakuri na sherehe za miaka 47 ya kuzaliwa kwa chama hiki muhimu kwa historia, umoja, uimara na maendeleo ya nchi yetu ziendelee kutusukuma mbele kuifanya vyema kazi iliyo mbele yetu; kazi ya kuhakikisha tunaipatia majawabu kila changamoto inayomkumba Mtanzania popote pale alipo kwa kiwango cha juu kabisa. Kidumu Chama Cha Mapinduzi. Kazi Iendelee.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live