Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Samia ataka mazungumzo mikutano ya kisiasa

Mikutano Ya Siasa Samia ataka mazungumzo mikutano ya kisiasa

Wed, 15 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ikiwa ni miaka mitano tangu Serikali ipige marufuku mikutano ya hadhara kwa wanasiasa, hatimaye leo Desemba 15, 2021 mwanga umeanza kuonekana katika suala hili ambalo limepasua ngoma kitaifa na kimataifa.

Katika utawala wa Hayati Magufuli, mwaka 2016 mapema tu mara baada ya kuchukua madaraka alianza kwa kuweka zuio la mikutano ya siasa ya hadhara kwa madai kuwa wawaache watu wafanye kazi.

Mapema hii leo, Rais Samia wakati akifungua mkutano wa wadau wa kujadili hali ya demokrasia ya vyama vya siasa nchini amewataka viongozi hao wa vyama vya siasa kujadiliana suala hilo vizuri na endapo mapendekezo yao yatairidhisha Serikali itaondoa zuio hilo.

Katika kufafanua hoja hiyo, Samia amesema kuwa ipo miongozo inayopaswa kutumika kwenye mikutano ya hadhara ikiwa ni pamoja na kufuata kanuni na sheria ya msajili wa vyama vya siasa pamoja na jeshi la Polisi.

Amekemea na kutaja baadhi ya tabia ambazo zilipelekea kusitishwa kwa mikutano hiyo na kuwataka viongozi wa vyama vya siasa kutumia haki hiyo ya kikatiba vizuri pasipo kuvunja sheria ya nchi.

"Kuna baadhi ya matendo ambayo yalipelekea kufungwa kwa mikutano ya hadhara, wala yasingefanyika isingefungwa, tatizo mnaichukulia vibaya mna fanya vurugu, mnavunja mali za watu, mnavunja sheria kila kukicha, hakuna atakayekubali mtafungiwa tu! Amesema Samia.

Ameongeza kusema kuwa suala hilo ni haki ya kikatiba hivyo wakae na kujadiliana njia sahihi za kufanya mikutano hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live