Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Samia ataka kanuni vyama vya siasa, atoa maagizo haya...

Samia Makazii Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania

Mon, 21 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais Samia amekiagiza kikosi kazi maalum cha kuratibu maoni ya wadau wa demokrasia ya vyama vya siasa pamoja na ofisi ya msajili wa vyama vya siasa nchini kuja na kanuni za pamoja za uendeshaji wa vyama vya siasa nchini.

Akizungumza mara baada ya kupokea taarifa ya kikosi kazi cha kuratibu maoni ya wadau wa demokrasia ya vyama vya siasa leo Machi, 21, 2022 Ikulu ya Jijini Dar es Salaam, Rais Samia amewataka kuja na kanuni za pamoja zitakazoongoza vyama vyote vya siasa ili kumaliza changamoto za kisiasa nchini.

Amesema kuwa kanuni hizo zitasaidia kuondoa siasa za chuki kwani kutakuwepo na usawa wa utendaji kwa vyama vyote vya siasa nchini ikiwa ni malengo ya kumaliza sintofahamu ya kisiasa iliyopo.

"Ni vyema kuwepo kwa kanuni na sera maalum za pamoja kwa vyama vya siasa vyote ambazo zitafuatwa ili kuboresha mwenendo wa siasa nchini"

"Nadhani ofisi ya msajili inazo hizo kanuni lakini mnaweza kuzipitia muone kama zinahitaji maboresho au kama hazipo basi mkae na vyama vya siasa mziweke ziwepo" Amesema Rais Samia.

"Na mkishamaliza basi muelekeze vyama vya siasa kuzifuta kanuni hizo" Amesema Rais Samia.

Pia, ametoa angalizo kwa wajumbe hao kuhakikisha kanuni hizo hazikandamizi maslahi ya vyama vya siasa.

"Naomba nitoe angalizo moja, kanuni hizi zisikandamize wala kuua vyama vya siasa bali zijenge na kuimarisha vyama" Amesisitiza Kiongozi huyo Mkuu wa Nchi.

"Haipendei kila siku tupo kwenye ma- CNN, BBC, Tanzania hivi, Tanzania vile, Hapana! Amesisitiza Kiongozi huyo Mkuu wa Nchi.

Aidha amesisitiza suala la elimu ya siasa ili kusaidia kuondoa mkanganyiko uliopo kwenye uendeshaji wa vyama hivyo na kuwataka viongozi wa dini, asasi za kiraia taasisi mbalimbali kusaidia zoezi hilo ikiwa ni pamoja na kuifundisha jamii juu ya umuhimu wa uzalendo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live