Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Samia asisitiza Watanzania kuichagua CCM

541fe0da65fd82c1953a97f02d235471 Samia asisitiza Watanzania kuichagua CCM

Sun, 20 Sep 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MGOMBEA mwenza wa kiti cha Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM),amiauluhu Hassan amesema watanzania wana kila sababu ya kuendelea kukichagua chama hicho, kutokana na mafanikio makubwa yaliyopatikana katika kipindi cha miaka mitano.

Samia alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki alipohutubia mamia ya wakazi wa mji wa Mbambabay Jimbo la Nyasa kwenye mkutano wa kampeni kwa ajili ya kumuombea kura Mgombea Urais wa CCM, Rais John Magufuli katika mkoa wa Ruvuma.

Aliwaomba wananchi wa jimbo la Nyasa kumpa Rais Magufuli miaka mitano mingine, ili aendelee kuleta maendeleo kama alivyofanya katika kipindi cha miaka mitano inayomalizika mwaka huu.

Alieleza kuwa mgombea huyo wa urais amefanya mambo mengi ya maendeleo yaliyoibadilisha wilaya ya Nyasa. Alisemaerikali ya CCM imewatendea haki wananchi kwa kuboresha sekta za afya, maji, usafiri, elimu, usafiri wa majini na barabara.

Alisema barabara ya lami kutoka wilaya ya Mbinga hadi Mbambay ni ushahidi tosha kwa wananchi hao.

Samia aliongeza kuwa kama wananchi wataendelea kukiamini Chama Cha Mapinduzi na kumpa ushindi wa kishindo Rais Magufuli, utakaomwezesha kuongoza nchi kwa miaka mitano mingine na kumaliza kero zilizobaki.

Aliwataka wanaCCM na wa vyama vya upinzani, kuwapigia kura wagombea wa CCM kutokana na sera nzuri za chama hicho zilizopo kwenye Ilani inayotekelezeka, tofauti na vyama vingine ambavyo vinaongozwa kama taasisi ya mtu binafsi

Alisema katika kipindi cha miaka mitano, serikali imewaletea wananchi maendeleo makubwa katika sekta zote, hivyo aliwaomba wakiamini kwa kukipa tena kura ili wafanye mambo makubwa zaidi.

Chanzo: habarileo.co.tz