Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Samia alivyokwenda Chadema nikajua anakwenda kuitumbukiza CCM - Musukuma

Msukuma Hj Musukuma akizungumza Bungeni

Wed, 5 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jana, Aprili 4, 2023 Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepitisha Azimio la kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuimarisha Demokrasia nchini na kukuza Diplomasia ya uchumi Bungeni jijini Dodoma.

Akichangia hoja hiyo, Mbunge wa Geita Vijijini amempongeza Rais Samia kwa kuboresha mfumo wa Demokrasia hapa nchini ambayo imeleta taswira halisi ya siasa ikiwa ni pamoja na kukuza uchumi wa nchi.

Musukuma amesema kuwa, Rais Samia ameonyesha ukomavu wake katika kazi kwani maendeleo yanaonekana kila idara katika jamii na kuongeza kuwa, mpaka kufikia wadhifa wa urais, maana yake amepitia mengi na amejifunza mengi pia.

"Mimi ni mmoja wa watu ambao nilimuangalia sana Mheshimiwa Rais siku anaenda kwenye mkutano wa Chadema Kilimanjaro, yani nilikuwa najiuliza hii CCM tunaenda kuitumbukiza wapi.

"Lakini baadae nilivyokuja kutafakari nataka niwaambie hivyo ndio maisha ya wanasiasa tunaishi, haya ndio maisha yetu wanasiasa mkituona tunazodoana na upinzani tukitokan nje tunanunuliana chai siyo Kama Aliyepita alivyotaka twende," amesema Musukuma.

Musukuma ameongeza kuwa kipindi Mama anakabidhiwa Urais kulikuwa na makundi mbalimbali kama Sukuma Gang na mengine mengi ila Rais hakujali hayo yote na akaendelea kuchapa kazi kama kawaida.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live