Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Samia aagiza kanuni mikutano ya kisiasa

23ae56bcb527fef01b44dc3d0a98cac6 Samia aagiza kanuni mikutano ya kisiasa

Sun, 13 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais Samia Suluhu Hassan amemuagiza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, Balozi Pindi Chana kuandaa kanuni zitakazoelekeza jinsi ya kufanya mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa.

Alitoa maelekezo hayo baada ya kupokea maazimio ya awali kutoka kikosi kazi alichokiteua cha kufuatilia hoja zilizojitokeza katika mkutano wa wadau wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa uliofanyika jijini Dodoma kuanzia Desemba 15 hadi 17 mwaka jana.

Rais Samia alimuagiza Waziri huyo kushirikiana na Tanganyika Law Society (TLS) pamoja na Zanzibar Law Society (ZLS) kutengeneza kanuni hizo.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, kikosi kazi hicho chenye wajumbe 24 na ambacho kinawajibika moja kwa moja kwa Rais, kiliwasilisha maazimio hayo Ikulu, jijini Dodoma. Maazimio hayo yamegawanyika katika makundi matatu ya muda wa utekelezaji.

Alisema azimio la muda mfupi ni uandaaji wa kanuni zitakazoelekeza jinsi ya kufanya mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa.

“Baadhi ya maazimio ya muda wa kati ni pamoja na rushwa na maadili katika uchaguzi, ruzuku, elimu ya uraia, huku masuala yanayohusu uchaguzi na katiba mpya vikiwa ni mpango wa muda mrefu,” alisema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live