Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Samia aachia neema hii Tabora

Samia Suluhu Hassan Kusini Samia aachia neema hii Tabora

Wed, 18 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

RAIS Samia Suluhu Hassan ameagiza kujengwa kwa vituo viwili vya Afya wilayani Nzega, sambamba na hayo ameagiza taa za barabarani zifungwe wilayani humo.

Rais Samia ameyasema hayo jana Oktoba 17, 2023 katika Uwanja wa Samora, wilayani Nzega, mkoani Tabora wakati akijibu maombi ya Mbunge wa Jimbo la Nzega na Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe kwa niaba ya Wananchi wa Jimbo hilo, yakiwemo ujenzi wa vituo vya afya, barabara kuwekewa taa pia ujenzi wa soko la kisasa kwa wajasiriamali mkoani Tabora.

“Hili jambo lifanyike kwa sababu Nzega ni kituo cha biashara na ujasiriamali, hivyo si vibaya vijana kufanya biashara saa 24 kwa yule atakayekuwa na nguvu ya kufanya hivyo. Kwahiyo taa ziletwe,

“Tukishakubali kujenga soko tutaangalia design inakuwa vipi ili kuwa na maegesho ya malori.” amesema Rais Samia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live