Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Salum Mwalimu wa Chadema akamatwa na polisi Iringa

31935 Mwalim+pic TanzaniaWeb

Mon, 17 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Jeshi la Polisi mkoani Iringa limemkamata Naibu Katibu Mkuu wa Chadema-Zanzibar, Salum Mwalimu.

Mwalimu amekamatwa leo Jumapili Desemba 16, 2018 Mafinga Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa akiwa anajiandaa kushiriki kikao cha ndani cha chama hicho kikuu cha upinzani nchini Tanzania.

Akizungumza na Mwananchi leo ofisa habari wa Chadema, Tumaini Makene amesema alikamatwa akiwa katika gari akielekea katika kikao hicho, akitokea Kanda ya Nyasa.

“Nimepata taarifa ya kukamatwa akiwa anaelekea kwenye kikao cha ndani Mafinga akitokea kanda ya Nyasa, kama mnavyojua tunaendelea na programu ya ujenzi wa chama ikiwemo ya Chadema ni Msingi,” amesema Makene.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa,  Juma Bwire alipotafutwa kutolea ufafanuzi tukio hilo amesema yupo kikaoni.

Endelea kufuatilia Mwananchi kwa taarifa zaidi



Chanzo: mwananchi.co.tz