Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Salama wa CUF aahidi makubwa Ukonga

Mon, 17 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mgombea wa ubunge wa CUF jimbo la Ukonga, Salama Masoud amesema hana utajiri wa kutumia magari kuomba kura bali atafanya hivyo kwa kutembea nyumba kwa nyumba.

 Akizungumza leo Septemba 15, 2018 katika mkutano wa  kufunga kampeni za ubunge wa jimbo la Ukonga, Salama amesema atanunua gari la wagonjwa ili kuwarahisishia wajawazito kufiki Hospitali mapema.

“Nitaishauri Serikali kuzitazama changamoto za barabara katika jimbo hili ili kurahisisha biashara za wananchi,” amesema.

Amesema atasimamia waendesha bodaboda kupewa semina maalum na kupata vibali vya kuingia katikati ya Jiji la Dar es Salaam.

“Mimi siwezi kuunga mkono Serikali kwa kuhama chama changu bali nitaishauri Serikali hasa katika ujenzi wa viwanda ili vijana wetu waweze kupata ajira kupitia chama makini  cha CUF,” amesema.

 “Nipeni kura jamani sio katika umahiri wa kuongea lakini nataka kutekeleza kile ambacho nimedhamiria kwenu.”

Amesema atapigania haki za kinamama bila kujali itikadi za vyama.

Chanzo: mwananchi.co.tz