Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sakaya ataka muswada ueleze utapunguza vipi ajali za bodaboda

39213 Pic+sakaya Sakaya ataka muswada ueleze utapunguza vipi ajali za bodaboda

Fri, 1 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Mbunge wa Kaliua (CUF) Magdalena Sakaya ametaka Muswada wa Sheria ya Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Ardhini wa mwaka 2018 kuelezea jinsi gani utakavyoweza kuwadhibiti waendesha bodaboda ili waweze kufuata sheria za barabarani.

Sakaya alikuwa akichangia miswada miwili ya Sheria ya Mamlaka ya Usafiri wa Ardhini wa mwaka 2018 na Sheria ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania wa mwaka 2018 leo Bungeni Jumatano Januari 30, 2019.

Amesema ajali nyingi za barabarani hivi sasa zinasababishwa na waendesha bodaboda ambao wamekuwa hawafuati sheria za usalama wa barabarani.

“Unakuta dereva bodaboda ana-overtake upande wa kushoto hawajui sheria za usalama wa barabarani. Ni jinsi gani muswada huu utadhibiti bodaboda ili kuokoa watu na ajali za barabarani,” amesema.

Amesema kuwa awali waliruhusu bodaboda kufanya biashara ya usafiri ili kuwawezesha vijana kuwa na ajira lakini imekuwa tofauti.



Chanzo: mwananchi.co.tz