Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sakata la Ndugai halijaleta mpasuko ndani ya chama- CCM

Ndugaipic Sakata la Ndugai halijaleta mpasuko ndani ya chama

Sun, 9 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

hama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kujiuzulu kwa aliyekuwa Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai hakuwezi kuleta mpasuko ndani ya chama hicho kwa kuwa kimeshawahi kupitia mitikisiko mingi lakini kikabaki imara.

Hayo yamesemwa leo Jumapili Januari 9, 2022 na Katibu Itikadi na Uenezi wa CCM, Shaka Hamdu Shaka wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi Kuu za CCM Kisiwandui Zanzibar, alipokuwa akijibu swali aliloulizwa kama ndani ya chama hicho kuna mpasuko.

Amesema kujiuzulu kwa Ndugai hakuwezi kuleta mpasuko kwa kuwa Chama hicho kimeshawahi kupitia mitikisiko ikiwamo baadhi ya viongozi wakuu wa chama hicho kuachia ngazi lakini lakini chama kikabaki imara.

Amesema “Yawezekana tukafikiria hili ambalo limetokea la kujiuzulu Spika wa Bunge na baadhi ya watu nimekuwa nikiwasikia wakikadiria kwamba eti ni sehemu ya CCM kupitia mpasuko kwa namna moja au nyingine, hakuna kitu kama hicho’’ amesema Shaka nakuongeza

“Hilo sio jambo la kwanza, kama mpasuko ungetokea mwaka 1984, mwaka 1984 lilitokea jambo kubwa la kihistoria, mwaka huo uliondoka muhimili mkubwa sana, Rais wa Zanziba wakati huohuo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mjumbe wa Kamati Kuu” amesema

Akitolea mifano ya baadhi ya viongozi waliowahi kujiuzulu, Shaka amesema “Kujiuzulu kwa Ndugai sio jambo la kwanza, Seif Sharif Hamadi (marehemu) na jopo lake waliachia ngazi alikuwa Waziri Kiongozi, Mkuu wa idara za CCM akiwa na wenzake saba ‘heavyweight’ waliondoka na chama kilibaki imara” amesema nakuongeza

“Sio hao tu, ukienda kweneye muhimili wa Serikali, ameondoka mzee Mwinyi wakati ule akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Edward Lowassa akiwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa hiyo kitabu cha historia ya CCM kina matukio ambayo ukitazama kwa haraka haraka unaweza ukasema CCM imemaliziaka lakini nataka niwaambie kumalizika kwa CCM kwa jambo moja ni kuja kwa nguvu mpya za kujipanga” amesema

Alhamisi Januari 6, 2022 aliyekuwa Spika wa Bunge, Job Ndugai alijiuzulu nafasi hiyo.

Katika taarifa yake kwa umma, Ndugai alisema “Naomba kutoa taarifa kwa umma wa Watanzania kuwa leo tarehe 06 Januari 2022 nimeandika barua kwenda kwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kujiuzulu nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri wa wa Tanzania na nakala yangu ya kujiuzulu nimeiwasilisha kwa Karibu wa Bunge” ilisema taarifa ya Ndugai ambaye ni Mbunge wa Kongwa

Muda mfupi baada ya taarifa ya Ndugai, Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo alithibitisha kupokea barua ya Ndugai ikimtaarifu kujiuzulu nafasi hiyo huku akibainisha kuwa utaratibu wa chama unaendelea wa kumpata Spika mwingine.

Leo, Shaka amemetangaza ratiba ya kuanza mchankato kumpata mwanachama atakayewakilisha chama hicho kugombea nafasi ya Spika wa Bunge la Tanzania akisema uchukuaji fomu utaanza Jumatatu Januari 10, 2021 na mwisho wa kurejesha itakuwa Januari 15, 2022.

Amesema fomu hizo zitatolewa Makao Makuu Dodoma, Ofisi Ndogo Lumumba Dar es Salaam na Afisi Kuu Kiwandui Zanzibar kwa gharama ya shilingi milioni moja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live