Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sakata la Mbatia, vita yahamia kwa Msajili wa Vyama

Mbatia Pic Data.jpeg James Mbatia

Thu, 26 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Uenezi wa Chama cha NCCR- Mageuzi Edward Simbeye amesema Msajili wa Vyama vya Siasa hana Mamlaka ya Kikatiba ya kumsimamisha Mwenyekiti wa Chama cha NCCR- Mageuzi kujihusisha na siasa.

Simbeye amesema James Mbatia bado ni mwanachama wa NCCR- Mageuzi na moja ya haki na majukumu ya mwanachama wa chama cha Siasa ni kufanya shughuli za chama hivyo ili Mbatia asifanye siasa inabidi asiwe mwanachama jambo ambalo Msajili wa Vyama vya Siasa hana Mamlaka nalo kikatiba la kumvua Mbatia Uanachama.

Simbeye ameendelea kwa kusisitiza kuwa barua hiyo iliyoandikwa kutoka kwa Msajili wa Vyama vya Siasa ni batili kwani inaonesha imeandikwa tarehe 25 Mei, 2021 lakini pia maudhui ya barua hiyo yanaonesha wazi kuwa Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa Sisty Nyahoza ametumia kujitetea kutokana na tuhuma zake za kudaiwa kutumika kuvivuruga Vyama vya Siasa.

Ameendelea kwa kusema kuwa kikao kilichoongozwa na Joseph Selasini ni kikao haramu na cha kihuni kwani Selasini si mwanachama wa NCCR- Mageuzi bali ni mwanachama wa Chadema na ushahidi wa barua upo kutoka Chadema Kata ya Makiidi Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro

ikionesha Joseph Selasini akitakiwa kujieleza kutokana na kusababisha vurugu katika Chama cha NCCR-Mageuzi.

Kwa mujibu wa barua hiyo Selasini amepewa siku 14 kujieleza kwanini asivuliwe uanachama wa Chadema kwa kosa la kutosema ukweli katika kujihusisha na migogoro ya vyama vingine vya siasa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live