Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sababu za Chadema kuandamana leo hizi hapa

Sababu Za Chadema Kuandamana Leo Hizi Hapa Sababu za Chadema kuandamana leo hizi hapa

Wed, 24 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, Chadema, kimefanya maandamano kukemea mapendekezo ya miswada ya sheria ya uchaguzi, gharama kubwa ya maisha na kucheleweshwa kwa marekebisho ya katiba.

Polisi wameruhusu chama hicho ufanya maandamano katika jiji la kibiashara la Dar es Salaam lakini wakaonya dhidi ya ghasia na uchochezi, vyombo vya habari vya ndani viliripoti.

Sababu za Maandamano

Katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Januari 13, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema maandamano yanalenga kuishinikiza Serikali kuzingatia maoni na mapendekezo ya wadau mbalimbali kuhusu masuala ya uchaguzi.

Vilevile chama hicho kinaitaka serikali iondoe Bungeni miswada inayohusu vyama vya siasa na uchaguzi, ambayo ni muswada wa Marekebisho ya Sheria za Vyama vya siasa na Sheria ya gharama za Uchaguzi.

Badala yake Serikali iwasilishe muswada wa kukwamua mchakato wa Katiba mpya kwa kuzingatia mwafaka wa kitaifa kwani Chadema inaamini, "serikali imepuuza maoni yaliyotolewa na Kikosi Kazi pamoja na wadau mbalimbali."

Kadhalika, Chadema imeitaka Serikali iwasilishe bungeni muswada wa kufanya marekebisho ya mpito ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ili uchaguzi wa serikali za mitaa wa 2024 na ule mkuu wa 2025 uwe huru na haki.

Suala la gharama za maisha pia limekuwa ajenda ya maandamano: "Tunataka serikali ipeleke mpango wa kuwakwamua wananchi na hali ngumu ya maisha Bungeni, ikiwa ni pamoja na kushusha bei ya bidhaa muhimu au kuweka ruzuku katika baadhi ya bidhaa," amesema Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live