Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sababu za ACT Wazalendo kutoshiriki uchaguzi Kinondoni na Siha

1676 DSC 2251 660x400

Mon, 22 Jan 2018 Chanzo: millardayo.com

Leo January 21, 2018 Chama cha ACT Wazalendo kimetangaza kutoshiriki uchaguzi wa Ubunge Kinondoni na Siha na Kata za Udiwani February 17, 2018 kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kutokuwepo uwanja mpana wa mapambano.

Akiongea na Waandishi wa Habari Naibu Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo bara Msafiri Mtemelwa amesema moja ya sababu ya kutoshiriki ni kutokana kuwepo kwa mapungufu katika chaguzi ndogo zilizopita ikiwemo baadhi ya viongozi wa umma kuingilia uchaguzi, jeshi la polisi na Wakurugenzi.

“Sisi ACT Wazalendo tunaendelea na kutoshiriki kwa sababu bado hatujapata uhakika wa uwanja wa mapambano, Tume ilikutana na wadau na walikiri na kusema wameanza kukemea Wakuu wa Wilaya na Mikoa wasishiriki,” -Mtemelwa

GOOD NEWS: TRENI KUTOKA DSM MPAKA RWANDA ITACHUKUA SAA 12

Chanzo: millardayo.com