Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sababu ya SUGU kukosa dhamana na kupelekwa rumande leo

1416 Sugu 640x400

Wed, 17 Jan 2018 Chanzo: millardayo.com

Mchana wa January 16, 2018 Mahakama ya Hakimu Mkazi Jijini Mbeya imeamuru Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyassa Emmanuel Masonga wapelekwe rumande mpaka January 19, 2018 kwa kesi ya uchochezi.

Hii ni baada ya Wakili wa Serikali Joseph Pande kuiomba Mahakama kutowapa dhamana kwasababu za kiusalama kwani kumekuwa na viashiria kuwa wawili hao wanafuatiliwa na hivyo usalama wao kuwa mdogo.

Wawili hawa wanashtakiwa kwa kutoa lugha za matusi dhidi ya Rais John Magufuli katika mkutano wa hadhara wa Mbunge Sugu uliofanyika December 30, 2017 katika viwanja vya shule ya msingi Mwenge jijini Mbeya.

Dr Tulia baada ya kusikia changamoto za watu wake Mbeya

Watu 7 kizimbani kwa kujiunganishia bomba la mafuta ya Dizeli



 

Chanzo: millardayo.com