Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sababu ya ACT-Wazalendo Serikali ya Umoja wa Kitaifa

Haji Juma Haji Duni, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo

Thu, 19 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha ACT-Wazalendo Juma Haji Duni amesema busara ndiyo inayokifanya chama chao kiendelee kubaki ndani ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) kwa masilahi ya wananchi.

Tangu ulipomalizika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Konde ambao chama hicho kilidai mgombea wao aliporwa ushindi kumekuwa na mvutano mkubwa ambapo baadhi ya viongozi na wanachama wa ACT-Wazalendo wakitaka waondoke ndani ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Amesema baada ya kikao cha dharura cha Kamati Kuu kilichoketi Agosti 8, mwaka huu, kiliagiza waendelee kubaki ndani ya SUK na kushiriki upya uchaguzi mdogo wa jimbo hilo kwa masharti maalumu.

Uchaguzi mdogo ulifanyika Julai 18 na Sheha Faki Mpemba wa CCM aliibuka mshindi kabla ya kujiuzulu nafasi hiyo kwa madai ya matatizo ya kifamilia.

"Ulikuwa ni mvutano mkubwa lakini busara ikaonekana tuendelee kuwa ndani ya SUK, maana ni haki ya Wazanzibar, Kamati Kuu liagiza tushiriki uchaguzi wa Konde ambao tayari Tume imeshatangaza jimbo hilo kuwa wazi"

Hata hivyo ilibainika kuwa hatua hiyo ilifikiwa baada ya uongozi wa chama kukutana na Rais Samia Suluhu Hassan na Dk Hussein Mwinyi kueleza matatizo yaliyotokea katika uchaguzi huo

Chanzo: www.tanzaniaweb.live