Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

SPIKA: Acheni siasa Rais anaupiga mwigi

Spika Wa B Spika wa Bunge akiwapa neno wananchi wa Rungwe kuacha siasa

Wed, 2 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson, amewaasa wananchi wa Tukuyu Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya kuacha kutumia muda mwingi kujadili siasa badala yake waelekeze nguvu na maarifa katika miradi itakayowaletea maendeleo.

Spika ameyasema hayo wakati wa Mkutano wa hadhara uliofanyika Wilayani humo kwa lengo la kumpongeza kuchaguliwa kwake kuwa Spika wa Bunge.

Pamoja na kuwashukuru wananchi hao kwa kujitokeza kwa wingi kwenye mkutano huo, Spika amemshukuru Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kusimamia mchakato wa kupitisha jina lake na kugombea nafasi hiyo.

“Hii nafasi tusingeweza kuipata bila yeye lakini shukrani zetu zinakwenda mbali zaidi ya hapo. Katika wingi wa mambo aliyoyafanya, sisi kama Wananchi wa Rungwe lazima tumshukuru kwa miradi mbalimbali inayoendelea katika maeneo yetu. Sekta ya elimu hapa ameleta zaidi ya shilingi billioni 1.1 ili madarasa yajengwe kwenye shule zetu za sekondari watoto wetu waweze kusoma. Rais wetu haupigi mwingi huko kwingine pekee bali anaupiga mwingi hadi hapa kwetu Rungwe” ameongeza Dkt. Tulia

Aidhaa, amewaeleza Wananchi hao kuhusu miradi mingine mbalimbali iliyofanywa na Serikali katika sekta ya afya na miundombinu, ambapo pia amewataka kuendelea kushikamana pasipokufuata mihemko ya kisiasa kwakuwa.

Kwa upande wake Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Mbeya kupitia CHADEMA Sophia Mwakagenda amesema kuwa licha ya tofauti zao za kichama lakini anampongeza Mhe. Spika pamoja na Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwakuwa wamekuwa ni Viongozi bora na wa mfano katika taifa na dunia kwa ujumla.

“W wewe ni Spika wa vyama vyote, mimi ni mmoja wa Wabunge wako ambao tulikuchagua kwa kura zote. Wakati tunakujadili tulisema hatuangalii chama bali tunaangalia akili na uwezo wa mtu” alisema 70460856 Mwakagenda

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Rungwe Ndg. Mpokigwa Mwankuga, amempongeza Mheshimiwa Dkt. Tulia kwa jitihada zake binafsi za kujitolea kwa jamii yake huku akitoa rekodi ya baadhi ya mambo aliyoyafanya ndani ya Halmashauri hiyo licha ya kwamba sio Mbunge wa eneo hilo.

“Katika rekodi ambayo Halmashauri hii imeweza kuzirekodi kwa wewe binafsi kujitolea katika sekta mbalimbali hadi sasa ni zaidi ya shilingi 1.13 bilioni Mheshimiwa Spika fedha hizi ungeweza kuzipeleka kwenye familia yako lakini uliamua kuwasaidia wana-Rungwe ili kuhakikisha wote wanapata maendeleo, tunakushukuru sana” alisema Mwankuga

Chanzo: www.tanzaniaweb.live