Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

SHILINGI BILIONI 331.7 KUTUMIKA KUKAMILISHA UCHAGUZI MKUU

Nec Logo?fit=800%2C445 SHILINGI BILIONI 331.7 KUTUMIKA KUKAMILISHA UCHAGUZI MKUU

Mon, 3 Aug 2020 Chanzo: zanzibar24.co.tz

Jumla ya shilingi Bilioni 331.7 zinatarajia kutumika katika kukamilisha Uchaguzi Mkuu utakofanyika Oktoba 28, 2020, ambapo fedha hizo zitatolewa na Serikali

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mstaafu, Semistocles Kaijage amesema fedha hizo zitatolewa kupitia Mfuko Mkuu wa Hazina kwa kuzingatia kifungu cha 122 cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, hatua iliyopongezwa kwa serikali kugharamia uchaguzi huo.

Jaji Kaijage ameongeza kuwa jumla ya wapiga kura milioni 29.2 wamejiandikisha kupiga kura za madiwani, wawakilishi, wabunge na Rais.Amesema kutokana na idadi hiyo ya wapiga kura, kutakuwa na vituo 80,155 vya kupigia kura na kila kituo kimoja kitahudumia wapiga kura wasiozidi 500.

Chanzo: zanzibar24.co.tz