Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

SHAKA: Dola hailindwi kwa marungu na mapanga

Shaka Pic Data Shaka akiwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Abdulrahman Kinana

Tue, 26 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimewataka wanachama wake kuhakikisha wanalinda dola kwa kufanya kazi na kutekeleza Ilani na ahadi zote wakati wa uchaguzi.

Kimesema kuwa wananchi ambao ndio wapiga kura zinazomuweka madarakani Rais, wabunge na madiwani ndio waajiri na wanaostahili kutumikiwa kikamilifu na hapo ndipo Chama kitaendelea kulinda dola na sio kwa silaha.

Akizungumza kwenye mkutano wa ndani wa wanachama wa CCM mkoani Kilimanjaro, Shaka amesema kamwe huwezi kulinda dola kwa kutumia silaha.

“Hamuwezi kulinda dola kwa marungu na mapanga, zaidi tunapaswa kutekeleza kwa vitendo yale yote tuliyoahidi wakati wa uchaguzi. Tunapofanya vizuri hapo tunakuwa na uhakika wa kuendelea kushika dola,” amesema Shaka.

Shaka ambaye ameongozana na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Kanali mstaafu Abdulrahman Kinana kwenye ziara ya kukagua uhai wa chama mkoani hapa, amewaambia wanachama wa chama hicho kuwa hakuna sababu ya kutofanya vizuri kwenye uchaguzi mkuu 2025.

“Hakuna sababu ya kukosea 2025 kwa sababu ya Rais tuliyenaye (Samia Suluhu Hassan) Mungu ametupa kwa ajili ya kutatua shida za wananchi. Mungu ametupa Kinana ambaye anakijua vyema chama na anamsaidia mwenyekiti (Rais Samia) kutattua shida za Watanzania,” amesema Shaka ambaye ametumia fursa hiyo kuwataka wananchi kupuuza uzushi kuhusu usafiri wa treni kati ya Dar es Salaam na Kilimanjaro.

“Kumekuwa na propaganda kuwa tangu ameingia Rais Samia huduma za treni zimesimama...huo ni uongo wa mchana kabisa. Nataka kuwaambia kuwa Serikali itafanya matengenezo makubwa ya njia ya treni na Chama tumeelekeza ikamilishe haraka matengenezo hayo.” amesema.

Amesema wananchi wa Kilimanjaro wawe tayari kusafirisha mazao yao nje ya nchi baada ya Rais Samia kufungua fursa mbalimbali za kiuchumi na baadhi yatatumia treni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live