Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

SAU yampitisha Mgaywa kugombea nafasi ya urais

F521e7c375afa4e4ed9918d8c9c6af8b.png SAU yampitisha Mgaywa kugombea nafasi ya urais

Wed, 29 Jul 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

CHAMA cha Sauti ya Umma (SAU) kimempitisha Muttamwega Mgaywa kuwa mgombea wake wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika nchini Oktoba 28, mwaka huu huku Satia Musa Sebwa kutoka Zanzibar akiteuliwa kuwa mgombea mwenza.

Akiwatambulisha wateule watakaogombea katika nafasi za urais Tanzania Bara na Visiwani (Zanzibar) kwa wanachama na viongozi wengine katika Mkutano Mkuu Maalumu wa Taifa wa chama hicho, Mwenyekiti wa SAU, Bertha Mpata alisema chama pia kimemteua na kumpitisha Issa Mohamed Zonga kutoka Zanzibar kuwa mgombea urais wa Zanzibar.

Aidha, Katibu Mkuu wa SAU, Majalio Kyara aliwataka wanachama kuwa na weledi na kwamba, siku ya uchaguzi wamalizapo kupiga kura, kila mmoja arejee nyumbani kusubiri matokeo ili kuepusha mikusanyiko kinyume cha sheria kwani inaweza kusababisha kuvunjika kwa amani.

Mteule wa kugombea urais kupitia SAU kwa Tanzania Bara, Mgaywa alisema kupitia uzoefu wake katika siasa, atasimamia maadili ya vyama wakati wote wa mchakato kwani SAU haipo kwa ajili ya upinzani tu, badala yake imelenga uamuzi unaofikiwa na chama hicho yaweze kufika Ikulu na kuleta mabadiliko.

Mgombea urais wa Zanzibar, Zonga na Sebwa ambaye ni mgombea mwenza, walisema watasimamia misingi yote iliyotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa na kuhakikisha wanasimamia misingi na ilani ya chama. Katika mkutano huo, Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa nchini, Sisty Nyahoza, aliwataka SAU kutojihusisha na vitendo vyovyote vya rushwa ili kulinda nidhamu ya chama chao.

Aliwataka watakaochaguliwa na NEC kuwa wagombea katika uchaguzi mkuu kufuata maadili ya vyama vya siasa na kukipongeza SAU kuwa mstari wa mbele kufuata taratibu, kanuni na maadili yanayopaswa kufanywa na vyama vya siasa

Chanzo: habarileo.co.tz